LHRC yazidi kuwajengea uwezo wasaidizi wa kisheria nchini.

Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini kimekutana na wasaidizi 64 wa kisheria kutoka katika wilaya 28 nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku ilikuwajulisha mabadiliko ya sheria na pia sheria mpya.

Kutaniko hilo huwa linafanyika mara kwa mara kila mwaka ikiwa ni kuwajengea uwezo wasaidizi hao ili kuwa watendaji bora katika maswala ya kisheria nchini, Pia kutaniko hilo lilikuwa na lengo la kumuaga  aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa kituo cha hicho Dr. Hellen Kijo Bisimba ambaye anamaliza muda wake kuwa Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho.

Bi Hellen akiongea amesema anafarijika kuona wasaidizi wa kisheria nchini wakiwa na shauku ya kuwasaidia watanzania katika maeneo mbalimbali nchini ili kupata msaada wa kisheria katika mazingira mbalimbali.

Bi Hellen aliongeza kuwa amezidi kufarijika kuona kuwa vituo hivyo vya msaada wa kisheria nchini katika wilaya mbalimbali vinazidi kuogezeka vikiwa na lengo la kuwasaidia watanzania katika maswala mbalimbali ya kisheria.

Baadhi ya wasaidizi wa kisheria kutoka Arusha na Manyara wamemwelezea Bi Hellen Kijo kuwa alikuwa msaada sana kwao katika kipindi chake hivyo hawata weza kumsahau,baadhi yao kwenda mbali zaidi kumwombea kwa Mungu afya nje na umri mrefu zaidi wa kuishi. 

Bi.Anna Henga ambaye ndiye mkurugenzi mpya wa kituo hicho cha sheria na haki za binadamu kwasasa ambaye amempokea kijiti Bi Hellen amesema amepewa dhamana kubwa ya kuendesha kituo hicho ila iko ndani ya uwezo wake hivyo amejipanga vizuri kuweza kutimiza majukumu yake kwa uwezo wote kwa kushirikiana na watendaji wake pia wasaidizi wa kisheria nchini kutimiza majuku ya kituo hicho.

Dr. Hellen Kijo Bisimba aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akizungumza na wasaidizi wa kisheria kutoka wilaya 21 nchini.
Bi.Anna Henga ambaye ndiye Mkurugenzi mpya wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akizungumza na wasaidizi hao wa kisheria nchini
Baadhi ya wasaidizi wa kisheria kutoka Arusha na ManyaraBaadhi ya wasaidizi wa kisheria kutoka Arusha na Manyara
Wasaidizi wa kisheria kutoka wilaya zote nchini wakifuatilia mafunzo kwa umakini
Wasaidizi wa kisheria kutoka wilaya zote nchini katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mkurugunzi wa Kituo hicho Dr.Hellen Kijo Bisimba na Mkurugenzi mpya Bi Anna Henga.
Wasaidizi wa kisheria kutoka wilaya zote nchini katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mkurugunzi wa Kituo hicho Dr.Hellen Kijo Bisimba na Mkurugenzi mpya Bi Anna Henga.

Post a Comment

Previous Post Next Post