Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu amewatoa hofu watumishi wa Taasisi zenye jukumu
la kulinda na kuhifadhi Wanyamapori na Misitu nchini kuwa hakuna maslahi
yao yatakayobadilika baada ya ujio wa Jeshi Usu
Naibu
Waziri Kanyasu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa
Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ikiwa ni mara yake ya kwanza
kukutana na watumishi hao tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa Naibu
Waziri katika Wizara hiyo nyeti kwa uchumi wa nchi.
Amesema
ziara yake imelenga kuzifahamu Taasisi anazoziongoza ili kujua namna
zinavyotenda kazi na changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi.
Akizungumza
kuhusu utendaji wa Jeshi USU, Naibu Waziri Kanyasu amesema kufuatia
mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka katika mfumo wa kiraia na kuwa
Jeshi USU kutakuwa na mabadiliko kiutendaji yatakayoendana na taratibu
za Jeshi USU lakini utakaoheshimu na kulinda maslahi ya watumishi.
Naibu
Waziri huyo ameeleza kuwa, uanzishwaji wa Jeshi hilo haukusudii
kubadili maslahi ya watumishi hao na endapo maslahi hayo yatabadilika
basi yatakuwa na mabadiliko chanya kwao.
Naibu
Waziri Kanyasu ameongeza kuwa Jeshi USU litaongeza nidhamu uwajibikaji
na maadili kwa watumishi wa sekta ya Maliasili na Utalii ili waweze
kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili na si vinginevyo.
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri Kanyasu ameiagiza Menejimenti ya Mamlaka
ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ibuni vivutio vipya vya Utalii
vitakavyosaidia kuongeza mapato kwa Serikali kwa kuzingatia majukumu
makuu ya Taasisi.
Kwa
upande wake, Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro,
Freddy Manongi amewahakikishia watumishi hao kuwa maslahi yao
hayatabadilika na ikiwezekana yataongezwa kwa sababu uwajibikaji
utaongezeka baada ya ujio wa Jeshi Usu
Ameongeza
kuwa mfumo wa Jeshi Usu haumaanishi kuwa Watumishi hawapaswi kupewa
maslahi yao na badala yake yanahitaji kuboreshwa zaidi ili waweze kuwa
na ari ya kufanya kazi katika kulinda Wanyamapori na Misitu nchini.
" Kati ya masuala ambayo nayapigania yasiweze kubadilika baada ya ujio wa Jeshi Usu ni maslahi yenu" amesema Dkt. Manongi.
Jeshi
USU lilizinduziwa rasmi tarehe 17 Novemba mwaka huu na Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan katika
Uwanja wa Fort Ikoma wilayani Serengeti mkoa wa Mara.
![]() |
| Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati alipowatembelea jana. |
![]() |
| Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana na Kanali Martin Kilugha mara baada ya kuwasili kati geti kuu la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro . |







