Kiongozi
huyo wa kanisa katoliki duniani ametoa kauli hiyo katika mahojiano na
Mmishenari kutoka Uhispania kuhusu wito wa kidini. Mahojiano hayo ni
sehemu ya kitabu kinachoandikwa na mmishenari huyo.
Papa
amesema mahusiano ya jinsia moja ni jambo la "fasheni", na ametaka
makasisi kutii viapo vyao vya utawa (kutojihusisha na mapenzi)
Gazeti la Corriere della Sera la nchini Italia limechapisha sehemu ya mahojiano hayo katika mtandao wake juzi Jumamosi.
Papa Francis amesema kanisa katoliki linapaswa kuwa "imara" wakati wa kuchagua watu watakaokua makasisi.
"Hili
suala la mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja ni kubwa sana," amesema
Papa na kusisitiza kuwa wale wote wanaohusika na mafunzo kwa makasisi
wahakikishe kuwa wanafunzi wao "wamekomaa kibinaadamu na kihisia" kabla
ya kuwapatia Sakramenti ya Upadre (upadrisho).
"Kwa sababu hiyo, Kanisa linawataka watu wenye tabia hizo (wapenzi wa jinsia moja) wasikubaliwe katika maisha ya ukasisi."
Agizo hilo pia linawahusu wanawake ambao wanataka kuwa watawa wa kanisa hilo.
"Katika
jamii zetu, sasa inaonekana kuwa suala hili la mapenzi ya jinsia moja
limekuwa fasheni. Mawazo kama hayo sasa yanaanza kupata ushawishi nadani
ya kasnisa," amesema papa na kuongeza: "suala hili katu halina nafasi
katika maisha ya watawa wetu."
Kuhusu
mahusiano binafsi ya Mungu na mtu mwenye kujihusisha na vitendo hivyo
alijibu; "Kama mtu ni shoga na anataka ukaribu na Mungu na ana nia
njema, mimi ni nani wa kuhukumu?"
"Nguvu
ya Utumishi", ni kitabu kilichotungwa na padre Fernando Prado,baada ya
mahojiano ya saa nne na Papa kuhusu changamoto za kuwa kasisi.
Kinatarajiwa kuchapishwa wiki ijayo.
CHANZO ; BBC SWAHILI
