Serikali kusaini mikataba na wamiliki wa Viwanda vya ubanguaji Korosho


Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa Kesho Januari 10 mwaka huu atasaini mikataba na wamiliki wa Viwanda vya ubanguaji wa Korosho waliojitokeza kwa ajili ya kubangua korosho za Serikali za msimu wa mwaka 2018/2019 zilizonunuliwa na Serikali kwa bei ya
Shilingi 3300 kwa kilo.

Waziri Hasunga ameyasema hayo Jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara.

Hasunga amesema kuwa Serikali ilitangaza kuwa korosho ghafi zote zitabanguliwa nchini hivyo utekelezaji wa jambo hilo umeanza, ambapo Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko itaingia mikataba ya ubanguaji.
 
"Tena nisisitize kwa wale wanaofanya biashara ya korosho kinyume na utaratibu maarufu
kama (Kangomba) wajisalimishe na kuomba radhi wenyewe kuliko kusubiri serikali
iwabaini” Alisema Hasunga
 
Pia amesema Wizara yake imeweka mikakati mbalimbali ambapo hadi kufikia Januari 31 mwaka huu zoezi la uhakiki wa wakulima wanaostahili kulipwa liwe limekamilika ambapo zaidi ya asilimia 80 ya wakulima wawe wamelipwa.
 



from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2C9xh4X

Post a Comment

Previous Post Next Post