Wakamatwa na Polisi kwa uwindaji haramu


watu watatu wanashikiliWA na Jeshi la polisi Mkoa wa Iringa kwa kutuhumiwa katika matukio ya uwindaji haramu maeneo ya hifadhi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Juma Bwire amewataja Watu hao kuwa ni Martine Kivike (41), Fred Kikobhe (32)Leonard Matelega (55).

Wamekutwa wanamiliki Magobore mawili, unga wa baruti wenye uzito wa gram 2 pamoja na vipande 15 vya nondo vilivyo chongwa mithili ya risasi baada ya kufanyiwa upekuzi shambani kwao ambao wamekiri kuhusika na uwindaji haramu.




Post a Comment

Previous Post Next Post