Breaking News

Kocha wa Singida United asimamishwa mechi tatu

Kocha wa klabu ya Singida United Dragan Popadic, amesimaishwa michezo mitatu baada ya kumzonga Mwamuzi wakati akitekeleza majukumu yake uwanjani.

Popadic aliondolewa kwenye benchi la ufundi wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Ndanda FC.

Kutokana na tukio hilo, Kamati ya Nidhamu ya TFF ilikaa na kujadili kisha kuja na maamuzi ya kumsimamisha jumla ya mechi hizo tatu.

Katika mchezo huo Ndanda FC ilifanikiwa kuitandika Singida jumla ya mabao 2-0, mechi ikipigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2Ud158M

No comments