Mechi zote za mwisho za robo fainali kuchezwa saa 1 Usiku
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limepanga mechi zote za mwisho za kuelekea robo fainali kuchezwa saa 1 za jioni.
Ratiba hiyo inawafanya Simba kushindwa kupanga ratiba ya mechi yake dhidi ya AS Vita Jumamosi kuchezwa saa 10 kama ilivyozoeleka.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema lengo la CAF kupanga ratiba hiyo ni kuepusha upangaji wa matokeo ambao wana hofu unaweza kujitokeza.
"CAF wameamua kupanga mechi zote za makundi kuchezwa saa 1 ili kuepusha upangaji wa matokeo", alisema Manara
Pia amesema mechi yao na AS Vita itapigwa saa 1 usiku na muda huo umepangwa na CAF na sio Simba.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2TtIXuV

No comments