Breaking News

Perez amesanda kwa Zidane

Real Madrid, baada ya kumtangaza kuwa kocha wao mpya wa sasa ni kocha wao wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane wengi wamefurahi sana na kuamini atakuja kuleta mabadiliko ndani ya kikosi cha Real Madrid, kila kukicha wamekuwa wakipata matokeo mabaya na mwendo wa klabu hiyo imekuwa sio mzuri sana.

Real Madrid, tatizo sio kocha tu tatizo Fiorentina Perez, amekuwa na nguvu kubwa kwa maana ya mamlaka kuliko makocha wake aliyowajiri.

Wachezaji wengi wa klabu hiyo umri umeshaenda na wameshinda mataji mengi makubwa ilikuwemo michuano mikubwa Barani Ulaya Uefa mara nne pia ikiwemo na mara tatu mfululizo.

Wengi wanaocheza kwenye kikosi cha kwanza wana miaka 30 na kuendelea Real Madrid , wanahitaji watumie pesa nyingi kwenye kuboresha kikosi chao ?ndio wanaweza kutumia hela nyingi kuwapata wachezaji je Fiorentina, hataweza kuvumilia kusubiri timu ingie ijengwe kwenye mfumo mpya?

Unaposajili wachezaji wapya katika timu inahitaji wazoeana kiutamaduni na hata kiuchezaji timu inapokuwa inatumia hela nyingi inakuwa kwenye presha kubwa sana inapocheza na Real Madrid, moja ya timu kubwa duniani.

Inawezekana kocha aliyeondoka alikuwa na mapungufu yake kwa kuwaacha Isco,na Marcelo kwenye kikosi cha kwanza na kupelekea timu kubadilika ghafla kiuchezaji?Isco moja ya wachezaji bora kabisa katika kikosi cha Real Madrid, tumemshuhudia chini ya Zidane akifanya makubwa Marcelo moja ya wachezaji bora katika idara beki wa pembeni.

Muda mwingine Fiorentina Perez, anahitaji kulaumiwa kwa kosa la kuingilia madaraka ya makocha na kutaka wachezaji anaowataka yeye ndo wasajiliwe kocha ndo mwenye maamuzi na kujua nani amfai nani anamfaaa katika mfumo wake?

Zidane nina imani kuwa kama atafanya usajili au kupewa fungu la pesa naamini Real Madrid, watarudi kwenye ubora na inahitaji uvumilivu wa hali ya juu.

Azizi Mtambo 15



from ShaffihDauda https://ift.tt/2CiUORY

No comments