Breaking News

Viongozi kwa viongozi kugombana ni ujinga - RC Simiyu


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amesema kuwa Viongozi kwa viongozi kugombana ni ujinga na kwake hilo haliwezi kutokea

Mtaka amewataka viongozi wenzake wenye mamlaka ya kufanya maamuzi katika maeneo ya kazi, watumie nguvu kubwa kujifunza kuliko kufanya maamuzi.

Myaka amesema hayo katika mdahalo kuhusu uongozi na maendeleo yenye tija kwa wote ulioendeshwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere mjini Bariadi.

Katika mkutano huo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na makatibu tawala wilaya zote mkoani humo wameshirikishwa.

"Viongozi kwa viongozi kugombana ni ujinga na kwangu haliwezi kutokea, wewe Mkuu wa wilaya au mkurugenzi una gari zuri, nyumba, mshahara mzuri, posho nyingi, maji, umeme kwa nini ugombane na mwenzako? Ni ujinga na haufai kuitwa kiongozi" Amesema Mtaka akiwakemea viongozi walio katika ugomvi.

"Tunamsumbua Rais, badala ya kumuacha aongelee mambo ya maendeleo ya nchi tunamfanya aongelee viongozi wanaogombana, anatumia muda wake kusuruhisha watu wanaogombana, hii ni kumdharau Rais, viongozi lazima tuheshimu nafasi za uongozi tulizochaguliwa na Rais wetu Magufuli," amesema Mtaka.

Aidha Mtaka alisema kiongozi lazima ajifunze kuliko kukimbilia kutoa matamko ambayo haya tija kwa wananchi.



from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2TxOQHh

No comments