Breaking News

DUH LIVERPOOL KWA REKODI NOMA, SASA WANOGESHA VITA YA UBINGWA DHIDI YA MANCHESTER CITY

USHINDI walioupata usiku wa Ijumaa  Liverpool wa mabao 5-0 dhidi ya Huddersfield uwanja wa Anfield umewafanya washushushe presha ya mashabiki pamoja na wachezaji ambao wapo kwenye kasi ya kuufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu England.
Naby Keita amefunga bao la mapema ndani ya Ligi Kuu England ndani ya sekunde 15 kabla ya Sadio Mane kupachika la pili dakika ya 23 na Mohamed Salah dakika 45, Mane alipachika bao lake la pili dakika ya  66 na Salah naye akamaliza kukamilisha mkono dakika ya 83 yanaifanya Liverpool kuwa na rekodi yake ya kipekee msimu huu kwenye ligi.
Mpaka sasa wanafanikiwa kuwa na wafungaji wawili ndani ya timu moja wenye mabao 20 ambao ni Mane mwenye mabao 2 huku Salah akifikisha jumla ya mabao 21 akiwa ni kinara kwa kucheka na nyavu.
 Kwa sasa vita yao inazidi kupamba moto na watetezi wa taji hilo, Manchester City ambao wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 89 wakiwa nyuma kwa mchezo mmoja huku Liverpool wakifikisha pointi 91.



from SALEH JEMBE

No comments