Breaking News

Mbunge aunga mkono kampeni ya Mama Samia


Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula ameunga mkono harakati ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan inayolenga uzazi salama na kupunguza vifo vya wajawazito yenye kauli mbiu "Tuwavushe Salama, Maneno sasa basi ni vitendo", kwa kutoa msaada wa vitanda vinne vya kujifungulia katika Zahanati ya Mhandu vyenye thamani ya Tsh. 11,200,000.00.

Mhe. Mabula amekabidhi msaada huo Leo kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kuwezesha Zahanati ya Mhandu kuanza kazi Mara moja kutokana na agizo la mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndg. John Mongella aliyetembelea Zahanati hiyo juzi.

Zoezi la makabidhiano limefanyika katika Zahanati hiyo na kuhudhuriwa na kaimu Mkurugenzi wa halmshauri ya Jiji la Mwanza ambaye ni Mganga Mkuu wa Jiji Dkt. Juma Rajabu Mfanga, Diwani Kata ya Mhandu Mhe. Constantine Sima, Mwenyekiti wa taasis ya First Community Ahmed Misanga, Katibu Mbunge Jimbo la Nyamagana Bi. Florah Magabe na Bi. Susan pamoja na Mtendaji wa Kata, wenyeviti wa Mtaa, viongozi wa CCM Kata.

from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2UGHJrI

No comments