Breaking News

TANESCO YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI WA MTWARA, LINDI WAKATI WA KIMBUNGA

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limewataarifu wateja wake wa Mikoa ya Mtwara na Lindi kuchukua tahadhari kutokana na taarifa ya uwezekano wa kuwepo kwa kimbunga katika mikoa hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu inasema  inawashauri wananchi kuwa mbali na miundombinu ya umeme, na iwapo kimbunga kitaambatana na mvua kutokujikinga chini ya nguzo ama transfoma ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Imesema iwapo mwananchi ataona miundombinu imeathirika kwa kuanguka ama waya kukatika, ni vema akatoa taarifa TANESCO huku ikizuia kushika wala kukanyaga waya uliokatika.

Pia iwapo kimbunga kitaambatana na tadi, upepo mkali, au umeme kuwa unapungua nguvu na kuongezeka ndani ya nyumba, unashauriwa kuzima umeme kwenye Main Switch hadi hali hiyo itakapotulia.


from MICHUZI BLOG

No comments