Rais wa Uturuki: Tutajenga hospitali mbili kwa ajili ya kukabilia na virusi vya corona
Rais wa Uturuki asema kuwa kutajengwa hospitali mbili mjini Istanbul kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona.
Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa umechukuliwa uamuzi wa kujenga hospitali mbili mabazo malengo yake ni kupambana na virusi vya corona.
Hospitali hizo zitajengwa mjini Istanbul.
Rais Erdoğan ameyafahamisha hayo baada ya kumalizika mkutano ambao uligubika na hatau ambazo zinastahili katika makabailaino dhidi ya Covid-19.
Rais Erdoğan ameendelea kufahamisha kuwa hatua nyingine zitaendelea kuchukuliwa iwapo itahitajika kwa kuwa hatua hizo malengo yake ni kupunguza na kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Hospitali mbili zitajengwa karibu na uwanja wa ndege wa Atatürk Yeşilköy na Sancaktepe, kila hospital moja itakuwa na vitanda 1000.
Ujenzi wa hospitali hizo unatarajiwa kumalizika baada ya siku 45.
Rais Erdoğan amesema kuwa idara ya afya imefanya kila liwezekanalo hadi kufikia idadi ya watu 20 000 kufanyiwa vipimo katika muda wa siku moja huku akiendelea kufahamisha kuwa matibabu baada ya kugunduliwa waathirika yatafanyika katika hospitali hizo mbili zinazotarajiwa ujenzi wake kumalizika baada ya siku 45.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2Xr4PIf

No comments