Kwanza, ni kuchoronga na kujenga njia ya kuchepusha maji ya mto ili
ili kupata eneo kavu katikati ya mto ili kuweza kujenga tuta kubwa
litakalohifadhi maji.
Hatua ya pili, ni kujenga tuta kuu la kuhifadhi maji.
Hatua ya tatu, ni kuchoronga na kujenga njia za kuporomosha maji ili yaweze kuzungusha vinu vya kufua umeme.
Hatua ya nne ni kujenga, kuunga na kusimika mitambo na vinu vya kufua umeme.
Hatua ya tano ni kujenga kituo cha kusafirisha umeme ili uweze kutumika katika gridi ya taifa.
Hatua
ya sita ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere
mpaka Chalinze ili kuingiza umeme kwenye gridi ya Taifa na kutumiwa na
wananchi.
Hatua ya saba ni ujenzi wa daraja la kudumu.
Hatua ya nane ni ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa mradi na barabara za ndani ya mradi.
#BwawaLetuLaNyerere #HatuaKubwaYaKihistoria #KuelekeaUmemeWaUhakika.

