DKT. SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA YA UONGOZI





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (PhD) katika uongozi. Tukio hilo limefanyika leo, tarehe 24 Novemba 2024, wakati wa sherehe ya mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, katika Kampasi Kuu ya Morogoro.

Heshima hiyo imetolewa kwa kutambua mchango mkubwa wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia katika uongozi, ikiwemo umahiri wake katika nafasi mbalimbali za utumishi ndani ya Chama, Serikali, na hata kimataifa. Mhe. Dkt. Samia pia alihudhuria kama mgeni maalum katika mahafali hayo yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Maekani.

Tukio hili limeonyesha namna mchango wa Rais Samia katika kuimarisha uongozi bora, kukuza maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kidemokrasia, unavyozidi kuthaminiwa, hiyo ikiwa ni shahada yake ya sita ya udaktari wa heshima kutunukiwa na vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post