Kafulila: Sheria ya ubia itaondoa changamoto kwenye miradi mingi
Uwepo wa Sheria ya Ubia ambayo inasimamiwa na kutekelezwa na Kituo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), kumetajwa kuwa kutasaidia kusimamia miradi mbalimbali nchini na kuondoa changamoto nyingi ambazo hapo awali zilikuwa zikijitokeza kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila amesema miradi mingi inachukua muda kukamilika kutokana na kuendelea kwa mazungumzo ili kuwa na miradi bora.
Amesema kwa sasa kuna miradi zaidi ya 60 iliyo chini ya utaratibu wa ubia kati ya sekta binafsi na serikali na ipo katika hatua tofauti tofauti ikiwepo mradi wa ujenzi wa barabara ya haraka ya Kibaha mpaka Chalinze yenye urefu kilomita 78.9 unaogharimu zaidi ya shilingi billion 700.
No comments