#KAZIINAONGEA

Katika kuendeleza dhamira yake ya kila Mtanzania kufaidika na rasilimali za nchi yake, Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kufanya maboresho ya kiuongozi kwenye mashirika mbalimbali ya umma.

Novemba 11,2024 amemteua  Mhandisi Peter Rudolf Ulanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Mhandisi Peter Ulanga, amechukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amemaliza muda wake.

Pia Rais. Dkt. Samia amemteua Prof. Harun Jeremia Mapesa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambapo kabla ya uteuzi huo, Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Prof. Mapesa anachukua nafasi ya Prof. Shadrack Mwakalila ambaye amemaliza muda wake.

#KAZIINAONGEA