SERIKALI YA RAIS SAMIA YABORESHEA WANANCHI BUSTANI YA UTALII TABORA
#KAZIINAONGEA
Kila Mtanzania anayo haki ya kufurahia rasilimali za nchi yake na katika kulifanikisha hilo Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi Millioni 220 kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa ajili ya kuboresho miundombinu ya utalii ndani ya bustani ya wanyamapori hai iliyopo mkoani Tabora.
Miundombinu iliyoboreshwa ndani ya bustani hiyo ni jengo la wananchi kupata taarifa za vivutio vya utalii vinavyopatikana katika bustani hiyo na Kanda ya Magharibi Kwa ujumla (Visitors Information Centre - VIC), vyoo vya kisasa kwa ajili ya wageni na mabanda ya wanyamapori walao nyama (Simba, Chui, Duma)
Maboresho hayo pia yameongeza tija katika makusanyo ya mapato, ambapo kabla ya maboresho TAWA ilikuwa inakusanya Tsh Millioni 1 kwa mwaka, lakini baada ya maboresho sasa wanakusanya kiasi kisichopungua Tsh Millioni 50 kwa Mwaka.
*#KAZIINAONGEA*
SERIKALI YA RAIS SAMIA YABORESHEA WANANCHI BUSTANI YA UTALII TABORA
Reviewed by Tanzania Yetu
on
December 16, 2024
Rating: 5
Reviewed by Tanzania Yetu
on
December 16, 2024
Rating: 5

No comments