JK Ahudhuria Kuapishwa Kwa Rais Mpya Wa Namibia Netumbo Nandi-ndaitwa
Na Mwàndishi Wetu
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
alikuwa miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria hafla ya kuapishwa
kwa Rais mpya wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah, iliyofanyika leo
tarehe 21 Machi 2025 katika jiji la Windhoek.
Katika
picha ya pamoja iliyopigwa mara baada ya tukio hilo la kihistoria, Dkt.
Kikwete anaonekana katikati, huku pembeni kulia kwake akiwa ni
mwenyeji wake – Rais mpya Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah.
Kushoto
kwa Dkt. Kikwete ni Jenerali Epaphras Denga Ndaitwah, ambaye ni mume wa
Rais mpya – akiweka historia kama “First Gentleman” wa kwanza katika
historia ya Namibia.
Kushoto
kwa picha hiyo ni Rais aliyemaliza muda wake, Mhe. Nangolo Mbumba,
aliyehudhuria hafla hiyo na kukabidhi rasmi madaraka kwa mrithi wake.
Kulia kabisa ni Mama Sustjie Mbumba, mke wa Rais Mstaafu wa Namibia.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Namibia kupata Rais mwanamke, jambo
lililopokelewa kwa shangwe si tu ndani ya nchi hiyo, bali barani Afrika
kwa ujumla. Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan pia
alihudhuria hafla hiyo, na kushuhudia kwa furaha wakati Mwanamke mwenzie
akitwaa madaraka kwa mara ya kwanza nchini humo, kama alivyofanya yeye
miaka minne iliyopita.
Tanzania
na Namibia zina historia ya muda mrefu ya uhusiano wa kindugu na
kidiplomasia, hususan kuanzia enzi za harakati za ukombozi wa kusini mwa
Afrika.
No comments