WASIOENDELEZA ARIDHI KWA MIAKA 3 KUNYANG'ANYWA, SHERIA YA ARIDHI KUTUMIKA
Na mwandishi wetu, Dodoma
Serikali imewaagiza wananchi wenye hati kuendeleza maeneo yao kwa kujenga kwani bila ikifika miaka mitatu sheria inawaruhusu kufuta hati zao na kuchukua kuwa mali ya serikali,
Hayo yamesemwa na Waziri wa Aridhi na maendeleo ya makazi Dk leonard akwilapo februari 12 wakati wa ufungaji wa siku kumi na nne za kliniki ya aridhi ambayo imefanyika mkoani jijini Dodoma.
Waziri akwilapo amesema sheria ya aridhi inamtaka mwenye hati kuendeleza aridhi ndani ya miaka mitatu kwa kujenga kilichokusudiwa na sio kujenga ukuta wala kibanda cha mlinzi.
Katika zoezi la kliniki hiyo jumla ya wananchi 4597 wamehudumiwa na hati 1598 pekee ndizo zilizochukuliwa na kuwaomba wananchi kuja kuzichukua hati zilizosalia kwani kuna jumla ya hati 2370 ambazo zipo ofisini hapo hazijachukuliwa .
Katika hatua nyingine waziri Akwilapo ametangaza wiki ya samia aridhi wiki ambayo ni maandalizi ya siku ya wanawake duniani ambapo amesema ofisi za aridhi watahudumia wanawake tu kuanzia tarehe 2 march tatu hadi tarehe 7 march 2026 ili kuwasaidia wananwake tu nchi nzima, ni katika kuwakomboa wanawake na masuala ya aridhi.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/zBcjWn7



No comments