Uteuzi wa Ummy ulitangazwa Juni 2, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusiluka kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bakari Machumu ukimrejesha katika eneo la afya ambalo amekuwa akilihudumia kwa miaka kadhaa akiwa serikalini.Waziri wa zamani wa Afya, Ummy Mwalimu amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa imani aliyompa huku akiahidi kutekeleza majukumu yake kwa weledi, bidii na uaminifu.
Ummy ametoa shukurani hizo ikiwa ni siku sita baada ya kuteuliwa kuwa Mshauri wa Rais wa masuala ya afya ya uzazi, mama na mtoto.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa Instagram leo Juni 8, 2026 na kuweka taarifa ya Ikulu ya uteuzi wake, Ummy amesema anashukuru kwa baraka za Mwenyezi Mungu na kwa heshima kubwa aliyopewa na Rais Samia kupitia uteuzi huo.
“Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kuniteua kuwa Mshauri wake wa masuala ya afya ya uzazi, mama na mtoto,” ameandika Ummy.
Mbunge huyo wa zamani wa Tanga Mjini amesema atatumia nafasi hiyo kutekeleza wajibu wake kwa kuzingatia dhamana kubwa aliyopewa Rais Samia, ambaye pia ametambuliwa na viongozi wa Afrika kama kinara wa afya ya mama na mtoto wa Umoja wa Afrika (African Union Champion for Maternal and Child Health).
Katika ujumbe huo, Ummy pia amewashukuru watu mbalimbali waliomtumia salamu za pongezi na kumuombea mafanikio baada ya uteuzi wake.
Uteuzi wa Ummy ulitangazwa Juni 2, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusiluka kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu ukimrejesha katika eneo la afya ambalo amekuwa akilihudumia kwa miaka kadhaa akiwa serikalini.
Kabla ya uteuzi huo, Ummy aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika Serikali ya awamu ya tano na ya sita.
Mwaka 2015 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Afya mwaka 2017 ambako alihudumu kama Waziri wa Afya hadi mwaka 2024.
Na Mwananchi Digital
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/ZriJWYx
Tags
News
