TANESCO yatangaza katizo la umeme utekelezaji mradi wa KV 400


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa utekelezaji wa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma unaendelea vizuri na umefikia zaidi ya asilimia 89.Kwa sasa, mkandarasi anaendelea na hatua muhimu ya kuvuta waya kwenye njia hiyo ya kusafirisha umeme. 

Ili kuruhusu kazi hizi kufanyika kwa usalama na ufanisi, kutakuwa na katizo  la meme kwa muda katika baadhi ya mikoa ya Morogoro na Tanga  kuanzia tarehe 9 hadi 14, 2026 kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

Hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa mradi unaolenga kuimarisha mfumo wa usafirishaji wa umeme nchini na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na wenye kuaminika kwa wateja.

          

Post a Comment

Previous Post Next Post