MUME WA RAIS SAMIA, HAFIDH AMEIR AFARIKI DUNIA




Na Mwandishi wetu,ZANZIBAR.

Mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan, Hafidh Ameir Hassan, amefariki dunia leo Jumatatu, Septemba 7, 2026.

Taarifa ya msiba huo imetolewa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, akisema Hafidh Ameir Hassan amefariki dunia majira ya saa mbili asubuhi katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, Zanzibar, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

“Ndugu wananchi, kwa masikitiko makubwa, ninawajulisha taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Hafidh Ameir Hassan, mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan,” amesema Ndejembi.

Makamu wa Rais ametoa pole kwa Rais Samia, familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu, pamoja na Watanzania wote kutokana na msiba huo.

Amesema mipango ya mazishi ya marehemu Hafidh Ameir Hassan inaendelea kufanyika Kizimkazi, Zanzibar, ambako familia inatarajiwa kuandaa taratibu za mwisho za mazishi.

Kifo cha Hafidh Ameir Hassan kimekuja wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiendelea kutekeleza majukumu yake ya kitaifa, huku taarifa hiyo ikisababisha simanzi miongoni mwa Watanzania na viongozi mbalimbali.

Malunde.com inaungana na familia ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.




from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/Dqla1Uw

Post a Comment

Previous Post Next Post