Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limetoa maagizo matatu kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na kuhama maeneo ya mabondeni, kusafisha mitaro, kuepuka ukataji miti kiholele sambamba na Utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwa ni tahadhari za mvua za El niño zinazotarajiwa kunyesha nchini.
Wito huo umetokewa na Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria (NEMC) Bw. Elibariki Bajuta wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili iliyofanyika tarehe 28 na 29 Septemba 2026 iliyoongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe mhandisi Hamad Yusuf Masauni iliyolenga kukagua maeneo yenye hatari ya kukumbwa na mafuriko na hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Mvua za El niño Mkoani humo.
Akizungumza na wananchi mara baada ya ziara hiyo, Mhe. Waziri Masauni Hamad Masauni
amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha wananchi wanaishi katika Mazingira salama dhidi ya maafa huku akizitaka Taasisi ushirikishwaji wa Jamii wakati wa ujenzi wa miundombinu kama vile mifereji na makaravati ili kuepusha migogoro ya ardhi.
Aidha, Mkurugenzi Bajuta amesisitiza wananchi kudhibiti matumizi ya Mifuko ya plastiki ambayo inachangia Kwa kiasi kikubwa kuziba Kwa mitaro ya kupitisha maji.
Maeneo yaliyokaguliwa katika ziara hiyo ni pamoja na eneo la ujenzi wa tuta la Reli ya SGR katika eneo la Mkundi hadi Lukobe, Mto Diwale (Kata ya Kichangani - Turiani), Eneo la Dumila (Mto Kikundi), Mto Mkondoa- Kidete Kata ya Kasiki pamoja na mto Mto Lumemo- Halmashauri ya mji wa Ifakara huku ikishirikisha TRC,Bodi ya Maji ya Bonde, TARURA, TANROAD, pamoja na Halmashauri za Morogoro mjini, Kilosa, Mvomero na Ifakara.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/Z0HoUcD
Tags
News









