RABIA ACHANGIA SH MILIONI 12 KWA WAHANGA WA MOTO MACHINGA COMPLEX DODOMA

 



Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalla Hamid (MCC), ametoa mchango wa Sh milioni 12 kwa wahanga wa moto ulioteketeza vibanda vya wafanyabiashara katika Soko la Machinga Complex, Jijini Dodoma.

Mchango huo umetolewa leo, Septemba 23, 2026, wakati Rabia akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Dodoma, ambapo amepokelewa katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma, kufanya kikao na Kamati ya Siasa pamoja na kutembelea vikundi mbalimbali vya wajasiriamali.

Katika ziara hiyo, Rabia pia amekutana na makundi mbalimbali ya kijamii, yakiwemo viongozi wa dini, wazee, machifu, wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, mafundi gereji, mafundi ujenzi, wanamichezo, wanafunzi wa vyuo, walimu, machinga, Mawinga, Mama Lishe, Baba Lishe, watu wenye mahitaji maalum, wajane na wagane.

Makundi mengine aliyokutana nayo ni vyama vya ushirika, maafisa usafirishaji pamoja na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali.

Akizungumza na wananchi, Rabia amesikiliza changamoto zinazowakabili na kutoa maelekezo ya utatuzi wa baadhi ya kero hizo papo hapo, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Amesema CCM itaendelea kushirikiana na wananchi katika kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zao, pamoja na kuhamasisha shughuli za uzalishaji na ujasiriamali kwa ustawi wa Watanzania.

Aidha, Rabia amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ana dhamira njema ya kuijenga Tanzania kwa maslahi ya Watanzania wote.




















from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/CAYFafd

Post a Comment

Previous Post Next Post