Na: OWM (KAM), Rukwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu amesema Serikali haiwezi kufanikisha maendeleo bila ushirikiano na taasisi za dini na kueleza kuwa uwepo wa taasisi hizo ni muhimili wa amani, utulivu na ustawi wa Taifa.
Mhe. Sangu amesema hayo tarehe 20 Septemba, 2026 katika harambee ya ujenzi wa nyumba za mapadre wa Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Kijiji cha Matai, Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.
Aidha, Ujenzi wa nyumba hizo utagharimu shilingi Milioni 93, katika harambee hiyo jumla ya mchango uliopatikana ni Shilingi 25,901,100 ambapo Mhe. Sangu amechangia kiasi cha Shilingi Milioni kumi.
Waziri Sangu, aliipongeza Parokia ya Matai kwa kufanikisha ujenzi wa Kanisa la Parokia hiyo, ameongeza kuwa huwo ni mfano wa mshikamano wa waumini na jamii katika kuchangia maendeleo ya kiroho na kijamii.
Kwa upande wake, Baba Paroko Leonardo Nkungwe wa Parokia ya Bikira Maria wa Fatima aliishukuru Serikali kwa namna inavyoshirikiana kwa ukaribu na taasisi za dini katika kuleta maendeleo na ustawi wa jamii.
Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Peter Lijualikali, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, alisisitiza mshikamano wa waumini na jamii katika kufanikisha miradi ya maendeleo, akibainisha kuwa ushirikiano huo ni chachu ya mafanikio ya miradi mikubwa ya kijamii na kiroho.
Awali, akisoma risala Diwani wa kata ya Mkowe Mhe. Chrispin Mwananyau Kwa niaba ya Parokia ya Matai ameeleza kuwa waumini na jamii wamejitoa kwa dhati katika ujenzi wa Kanisa la Parokia hiyo, mradi uliogharimu Shilingi Milioni 250 na sasa wanaendelea kushirikiana katika ujenzi wa nyumba za mapadre.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/vtGRZQ5
Tags
News









