TPDC YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI SHINYANGA KUHUSU MAFUTA, GESI ASILIA NA EACOP

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP-TPDC, Jumanne Mohamed, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka TPDC, Jenifa Mshanga, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na TPDC.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi, maafisa wa TPDC pamoja na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.

Na Sumai Salum – Shinyanga

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limewajengea uwezo waandishi wa habari mkoani Shinyanga kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, pamoja na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo, Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena mkoani Shinyanga, yakilenga kuongeza uelewa wa waandishi kuhusu shughuli zinazofanywa na TPDC, matumizi ya gesi asilia, mradi wa EACOP, fursa zinazotokana na miradi hiyo pamoja na wajibu wa jamii katika kulinda miundombinu ya Taifa.

Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, amesema waandishi wa habari ni wadau muhimu katika kuelimisha wananchi kuhusu miradi ya kimkakati ya Taifa, hivyo wanapaswa kutumia nafasi yao kutoa taarifa sahihi na zinazoeleweka kwa umma.

Lyamongi amesema waandishi wana wajibu wa kueleza manufaa ya miradi ya mafuta na gesi, ikiwemo EACOP, pamoja na kuhamasisha wananchi kulinda miundombinu yake.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi.

“Tunajua waandishi ni nguzo ya nne ya dola, hivyo nyie mkiongea vizuri, wananchi wataelewa na kulinda miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta,” amesema Lyamongi.

Amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi ili iwe sehemu muhimu katika kukuza uchumi wa Taifa na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Aidha, amewataka wananchi kutumia fursa zinazotokana na miradi hiyo kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi zitakazowanufaisha wao binafsi pamoja na jamii zinazowazunguka, huku wakishirikiana na Serikali kuhakikisha miradi hiyo inalindwa.
Matumizi ya Gesi Asilia

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano TPDC, Marie Msellemu, amesema warsha hiyo ni sehemu ya mkakati wa shirika kuwa karibu na wadau wake, hususan waandishi wa habari, ili kuwapatia uelewa kuhusu shughuli za mafuta na gesi asilia pamoja na miradi mikubwa inayotekelezwa nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu.

Amesema gesi asilia ni nishati yenye matumizi mbalimbali, ikiwemo majumbani, viwandani na katika vyombo vya usafiri, huku ikitoa unafuu wa gharama kwa watumiaji.

Msellemu amesema matumizi ya gesi asilia katika usafiri yanaweza kupunguza gharama kwa watumiaji ikilinganishwa na baadhi ya nishati nyingine.

“Kwa mtu anayetumia gari kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro anatumia gesi yenye thamani ya Shilingi 11,000 hadi 17,000, wakati gesi hii asilia gharama ya kilo moja ni Shilingi 1,500 pekee,” amesema Msellemu.

Amesema TPDC inaendelea na mikakati ya kuongeza matumizi na usambazaji wa gesi asilia nchini, pamoja na kukabiliana na changamoto za teknolojia na bajeti katika kupanua huduma hiyo.

Msellemu pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kupata taarifa sahihi kuhusu sekta ya mafuta na gesi, akisema ushirikiano kati ya TPDC na waandishi wa habari ni muhimu katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu sekta hiyo na fursa zinazopatikana.

Januari 2027 Mafuta Kuanza Kusafirishwa

Akizungumza kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP-TPDC, Jumanne Mohamed, amesema utekelezaji wa mradi huo unazingatia masuala ya mazingira na jamii, huku hatua mbalimbali zikichukuliwa kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza.
Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP-TPDC, Jumanne Mohamed.

Jumanne amesema matarajio ni kwamba ifikapo Januari 15, 2027, mafuta yataanza kuingizwa kwenye bomba na kusafirishwa kuelekea kituo cha Chongoleani mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa TPDC, mradi huo unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini na unahusisha shughuli za kijamii na kiuchumi zinazolenga kuhakikisha wananchi wanaoishi katika maeneo yanayopitiwa na mradi wananufaika.

Jumanne amesema katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, mradi huo umehusisha vijiji na mitaa 16, huku kaya 10 zilizoathiriwa na utekelezaji wa mradi huo zikilipwa fidia yenye thamani ya takribani Shilingi bilioni 1.8.

Waandishi Wapongeza Mafunzo

Kwa upande wao, waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo wamesema yamewapatia uelewa mpana kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, pamoja na miradi ya kimkakati kama EACOP.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru, ameishukuru TPDC kwa kuandaa mafunzo hayo, akisema yamewaongezea waandishi ujuzi na uwezo wa kuandika kwa ufasaha zaidi kuhusu masuala ya mafuta, gesi asilia na miradi inayotekelezwa nchini.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru.

Waandishi hao wamesema maarifa waliyoyapata yatawasaidia kutoa taarifa sahihi, zenye uwiano na zinazoeleweka kwa wananchi kuhusu miradi hiyo, fursa zake, masuala ya mazingira na wajibu wa jamii katika kulinda miundombinu ya Taifa.

Utafutaji wa Mafuta na Gesi Shinyanga

Katika mafunzo hayo, TPDC pia imeeleza shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Bonde la Eyasi-Wembere, linalohusisha maeneo ya Mkoa wa Shinyanga, ikiwemo Wilaya ya Kishapu.

Waandishi wameelezwa kuhusu umuhimu wa shughuli hizo katika kuongeza fursa za kiuchumi, kuibua uwezekano wa upatikanaji wa rasilimali za mafuta na gesi na kuchangia juhudi za Serikali za kutumia rasilimali za ndani kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Mafunzo hayo yamefanyika wakati Tanzania ikiendelea na juhudi za kuendeleza sekta ya mafuta na gesi pamoja na miradi ya kimkakati, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutumia rasilimali za ndani, kuongeza fursa za kiuchumi na kuchochea maendeleo ya Taifa.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo Septemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Karena, Shinyanga.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia yaliyoandaliwa na TPDC

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP-TPDC, Jumanne Mohamed, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP-TPDC, Jumanne Mohamed, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP-TPDC, Jumanne Mohamed, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP-TPDC, Jumanne Mohamed, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.
Kaimu Mratibu wa Mradi wa EACOP-TPDC, Jumanne Mohamed, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia, leo Septemba 4, 2026.

from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/FTGjs0Q

Post a Comment

Previous Post Next Post