KOM Schools, taasisi ya elimu iliyopo mjini Shinyanga inayojumuisha shule ya awali, shule ya msingi na sekondari, imetangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Best Private School (Shule Bora Binafsi) katika tuzo za MDAU SHUPAVU Awards – Shinyanga 2026, Season 2.
Tuzo hizo zimetolewa Oktoba 20, 2026, katika ukumbi wa Miligo Hall, mjini Kahama, mkoani Shinyanga, kwa lengo la kutambua na kuenzi mchango wa watu binafsi, taasisi na biashara zinazofanya vizuri katika sekta mbalimbali.
KOM Schools inatoa huduma za elimu kuanzia ngazi ya awali hadi sekondari, hivyo kuwapa wanafunzi fursa ya kupata elimu katika ngazi mbalimbali ndani ya taasisi hiyo iliyopo Shinyanga mjini.
Kutambuliwa kwa KOM Schools katika kategoria ya shule bora binafsi ni sehemu ya utambuzi wa wadau wa elimu wanaoshiriki katika sekta muhimu ya maendeleo ya jamii.
MDAU SHUPAVU Awards zimeandaliwa na Taasisi ya HOLYSMILE, chini ya Mkurugenzi wake, Arnold A. Bweichum Jr, kwa lengo la kutambua juhudi, ubunifu na mchango wa wadau mbalimbali katika maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.
Washindi wa tuzo hizo walipatikana kupitia kura za wazi katika kategoria mbalimbali zinazohusisha elimu, biashara na ujasiriamali, habari, burudani, mitindo na urembo, ubunifu, uongozi na maendeleo ya jamii.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/QKqh5aH
Tags
News








