SERIKALI imesisitiza dhamira yake ya kuongeza kasi ya uunganishaji wa umeme nchini, huku ikitangaza hatua madhubuti za kuboresha miundombinu na kupunguza changamoto za gharama kwa wananchi wa vijijini na wenye kipato cha chini kupitia ushirikiano wa kimkakati na taasisi za fedha.
Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati akizindua rasmi utekelezaji wa makubaliano ya mpango wa ufadhili wa uunganishaji umeme kwa wananchi, uliotiwa saini kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Benki ya CRDB.
Ndejembi alibainisha kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kufikia zaidi ya wateja milioni sita waliounganishwa kwenye mfumo wa taifa, akisisitiza kuwa juhudi hizo zinaendana na malengo mapana ya Mission 300 ya kuongeza upatikanaji wa nishati kwa watu milioni 300 barani Afrika.
"Upatikanaji wa umeme hauhusiani na mwanga pekee, bali una mchango mkubwa katika kuongeza shughuli za kiuchumi, biashara, elimu, matumizi ya teknolojia na kuboresha maisha ya wananchi," alisisitiza.
Aidha, alibainisha kuwa Serikali inaendelea kuwekeza katika vituo vya kupokea na kusambaza umeme pamoja na njia za usafirishaji ili kuongeza uwezo wa mfumo. Hata hivyo, alisisitiza kuwa bado kuna haja ya kuwafikia wananchi wa vijijini ambao wanaweza kushindwa kumudu gharama za awali za kuunganishiwa nishati hiyo.
Kupitia uzinduzi huo wa makubaliano kati ya TANESCO na Benki ya CRDB, wananchi sasa wanapata njia rahisi na nafuu zitakazowawezesha kuunganishiwa umeme kwa wakati, huku kukiwa na wito kwa sekta binafsi na wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Serikali kufikia maono ya uchumi shindani na jumuishi.