Serikali
ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani inatarajia kutoa eneo kwa ajili ya
kujenga ukumbi utakaotumika kuwapatia mazoezi ya ngumi vijana wa wilaya
hiyo.
Aidha
imempongeza bondia Dulla Mbabe mzawa wa wilaya ya Kisarawe kwa ushindi
alioupata dhidi ya mpinzani wake Fransis Cheka lillilofanyika hivi
karibuni.
Hatua
hiyo ya kupatiwa eneo hilo imetokana na bondia huyo kutoa kauli ya
kutaka kutoa mafunzo kwa vijana wa kisarawe ili waweze kujifunza mchezo
huo. Akizungumza
kuhusu mpango huo Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo
amesema,Mbabe amewatendea haki kwa kushinda pambano lililofanyika
Desemba 26 mwaka uliopita dhidi ya Cheka.
Jokate alieleza, Kisarawe imejaa vipaji sio tu mpira wa miguu bali katika michezo mbalimbali. Aliahidi serikali ya wilaya kumpa uahirikiano kuhakikisha kipaji chake kinakua na kuibua vijana wengine.
Nae bondia huyo Mbabe alijigamba kwa kasema amecheza mipambano zaidi ya 20 ikiwemo ya kimataifa. Hata
hivyo aliwaahidi watanzania kufanya vizuri katika Mchezo wa kimataifa
unaokuja ambao unatarajiwa kufanyika mwezi march mwaka huu.
Katika
hatua nyingine mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Zainab Vullu,
alimhakikishia bondia huyo, wabunge wa mkoa huo watamkaribisha Dodoma
katika bunge ili kumtambulisha na kuitambulisha Kisarawe kuwa
inawanamichezo lukuki sio tu wa mpira wa miguu bali na masumbwi.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akimpongeza Bondia Dulla Mbabe,ambaye ni mzawa wa wilaya ya Kisarawe kwa ushindi alioupata dhidi ya mpinzani wake Fransis Cheka lillilofanyika hivi karibuni.
NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE

