| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akishuhudia utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula
Duniani (WFP) kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam
leo Ijumaa Januari 4, 2019. Walioketi kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa
WFP nchini Bw. Michael Dunford, Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent
Bashungwa na Dkt Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias
Kuandikwa. |