Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amewasili mji mkuu wa Beijing katika ziara yake ya siku nne nchini China.
Kulingana na shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA, Kim Jong Un na mkewe Ri Sol-ju wamewasili mjini Beijing ndani ya treni binafsi majira ya asubuhi.
Kim Jong Un amesindikizwa na kiongozi anayehusika na mazungumzo ya nyuklia na Marekani,Waziri wa mambo ya je wa Korea Kaksazini Ri Yong Ho na waziri wa ulinzi No Kwang Chol.
Shirika la habari la China la Shinhua pia limethibitisha kuwa Kim Jong Un na mawaziri wake tayari wamewasili mjini Beijing .
Kim Jong Un anatarajia kukutana na rais wa China Xi Jinping katika ziara yake hiyo ya siku nne.
Wakati wa ziara hiyo, mazungumzo ya amani kati ya Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini na mazungumzo na Marekani ya kuondolewa kwa silaha za nyuklia kutoka Peninsula ni kati ya mada zitakazojadiliwa.
from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2GXfpjk

Tags
News