Timu ya KMKM wameibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Chipukizi, kundi A kombe la Mapinduzi.
Mchezo huo umepigwa katika Uwanja wa Amani stadium majira ya Saa 10:15 jion.
Wafungaji katika mchezo huo salum Akida Dakika 70, Ibrahimu khamisi Dakika 90 pamoja na juma Ali dakika 84.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo kocha wa timu ya KMKM Ame Msimu, alisema wanashukuru mungu kwa kumaliza mchezo vizuri ila kwa sasa wanasubiri matokeo ya mchezo wa usiku ili wao wapite.
" Japo Mlandege ndugu zetu ila tunawaombea wafungwe ili kwetu sisi tupite na kuendelea hatua inayofuata" alisema kocha.
Kwa upande wa manager wa Timu Chipukizi Mohamed Abasi aliwaomba mashibiki wa timu hiyo kuwa wavumilivu licha ya timu kotofanya vizuri katika mashindano hayo.
Kombe la Mapinduzi linaendelea tena Usiku majira ya Saa mbili na robo kati ya Simba na Mlandege.
from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2sfKmoE
Tags
News

