Kocha Zahera afunguka kuhusu Makambo

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunga akidai kwenye mzunguko wa pili mshambuliaji wake Herieter Makambo atakuwa na mato zaidi ya mzunguko wa kwanza kutokana na kuanza kupata uzoefu wa Ligi ya Tanzania Bara.

Makambo kwa sasa ni kinara wa kupachika mabao akiwa na mabao 11 akifuatiwa na Said Dilunga wa Ruvu Shooting ambaye ana mabao 10 kwa sasa.

Zahera amesema kwa namna ambavyo anatambua uwezo wa Makambo, atafanya makubwa zaidi ya aliyofanya kwa sasa kwani anatambua vema namna ambavyo mshambuliaji wake anafanya akiwa eneo la hatari ama nje ya hatari.

"Wengi wananibeza ninapozungumzia uwezo wa Makambo hasa kwenye kufunga, ninamtambua katika kila hali hivyo sina mashaka naye, imani yangu atafunga mabao mengi zaidi ya aliyonayo sasa," alisema.

Yanga ni vinara wa Ligi wakiwa na pointi 50 baada ya kucheza michezo 18 na kufunga jumla ya mabao 35 wanashikilia rekodi ya kutopoteza mchezo mmoja mpaka sasa.

from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2C7r0GU

Post a Comment

Previous Post Next Post