Tanzania Prisons yaizimisha Mtibwa Sugar

Kikosi cha Tanzania Prisons kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Mabao ya Prisons yalifungwa na Salum Kimenya dakika ya 71 na bao la pili lilifungwa na Jumanne Elifadhili dakika ya 88 kwa mkwaju wa penati.

Matokeo hayo yanaifanya Prisons ifanikiwe kuvuna pointi tatu muhimu na kufikisha jumla ya pointi 15 baada ya kucheza michezo 20.




from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2RfZUba

Post a Comment

Previous Post Next Post