Serikali ya Mkoa wa Mjini yatoa ushauri kwa Wizara ya afya
Na. Thabit Madai Zanzibar
Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja imeishauri Wizara ya Afya kuwa na mipango mizuri ya utekelezaji wa huduma za afya katika ngazi ya serikali za mitaa ili hatua ya ugatuzi wa madaraka ifanikiwe ipasavyo.
Akizungumza jana wakati ufunguzi wa mkutano wa kutathmini huduma za afya visiwani humu uliowashirikisha wadau wa sekta ya afya Mkuu wa mkoa Ayoub Mohamed Mahmoud dhana ya ugatuzi katika sekta ya afya itaweza kufikiwa ikiwa kutakuwa na ushirikiano kati ya wizara ya afya,na Serikali za Mitaaa.
Mkuu huyo wa mkoa ameipongeza Wizara ya Afya na washirika wa maendeleo kwa juhudi kubwa walizochukua katika kuinua sekta ya afya visiwani humu pamoja na kupunguza magonjwa ikiwemo malaria na maambukizi ya ukimwi.
Alisema serikali ya mkoa huo ina tambua na kuthamini mchago unaotolewa na washirika wa maendeleo na kwamba wanapaswa kuendelea kuunga mkono jitihada za sekta hiyo ya afya.
Mbali na hilo, RC Ayoub amesifu juhudi zinazofanywa na Wizara ya afya katika kupunguza vifo vya mama na mtoto pamoja kuimarisha utoaji wa huduma katika eneo hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Jamala Adam Talib alisema dhamira ya mkutano huo ni kutathmini huduma za afya na kuweka mipango ya utekelezaji kwa mwaka 2019-2020 kwa kuzingatia mahitaji.
"Maradhi yasio ya mambukizi kama sukari na presha si nzuri hivyo serikali ina mpango wa miaka mitano ya kupunguza matatizo hayo,"alisema
Naye Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) kwa upande wa Zanzibar Dk. Ander michael alisema Shirika hilo litaendelea kutoa ushirikiano ili kuinua sekta hiyo muhimu kwa jamii.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2VmYxEZ
No comments