Breaking News

ISHU YA JUMA NYANGI WA ALLIANCE HAIJAMUACHA SALAMA, TFF YAMLAMBA FAINI NA MECHI TATU MFULULIZO



KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Ofisa Habari wa TFF, imetangaza kumfungia mechi tatu mchezaji wa Alliance Juma Nyangi pamoja na faini ya milioni mbili.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amesema Kamati hiyo imefikia maamuzi hayo baada ya mchezaji huyo kulalamikiwa kumtendea kitendo cha udhalilishaji mchezaji wa Yanga Gadiel Michael

Nyangi alimtendea kitendo hicho Gadiel  katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba na kumalizika kwa Yanga kushinda kwa bao 1-0.

Licha ya adhabu hiyo kutolewa, Nyangi aliitwa kwenye kamati kwa ajili ya mahojiano wiki kadhaa zilizopita na kukiri kuwa alitenda kosa hilo kisha kuomba msamaha.

Hata hivyo Kamati hiyo imesema Nyangi na Alliance wanayo haki ya kukata rufaa kwani ipo wazi.


from SALEH JEMBE

No comments