Breaking News

Mbunge Mavunde awawezesha wajasiliamali Dodoma


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde ameviwezesha vikundi vya Wajasiriamali vya Vijana na wakinamama vifaranga vya kuku 23,000 aina ya Kuroiler na mabwawa ya samaki kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji mali na kujiimarisha kiuchumi ambapo gharama ya jumla yote ni Tsh 68,000,000 fedha inayotokana na mfuko wa Jimbo.

Mbunge Mavunde amekabidhi jana vifaranga hivyo na Mabwawa ya samaki yanayohamishika kwa Vikundi katika kata zote 41 za Jimbo la Dodoma Mjini ambapo Mstahiki  Meya wa Jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe alipokea kwa niaba ya madiwani wa Jiji la Dodoma ambao nao kila mmoja atawasilisha katika kata yake husika.

Mavunde pia alitumia fursa hiyo kuwaomba wanafuika wa miradi hiyo kuhakikisha wanatunza kuku na samaki hao ili kuleta tija katika kukuza uchumi wa wananchi kwa kuwa hivi sasa Dodoma kuna soko la uhakika la samaki na kuku kutokana na uwingi wa watu Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo,Mstahiki Meya Prof. Mwamfupe amempongeza Mbunge Mavunde kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo na kuahidi kusimamia miradi hiyo kwa karibu ili ilete tija na kubadilisha maisha ya wananchi kiuchumi.

from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2Vt87Ki

No comments