Breaking News

Idadi ya vifo kutokana na kimbunga yaongezeka Vietnam


Idadi ya watu waliopoteza maisha yao huko Vietnam kutokana na kimbunga cha Malove, ambacho kimeanza tangu jana, imeongezeka hadi 19.

Maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na kimbunga kilichokumba Quang Nam, moja ya majimbo ya kati, yaliharibu makazi mengi jana, kulingana na taarifa iliyotolewa na Kamati Kuu ya Usimamizi ya Kuzuia na Kudhibiti Maafa ya Asili.

Imeripotiwa kuwa miili ya watu 6 zaidi imepatikana , watu 19 wamefariki, na watu wasiopungua 64 hawajulikani walipo.

Imearifiwa kuwa viwanda, shule na sehemu za kazi vimefungwa kwa muda katika mkoa huo ambapo zaidi ya watu elfu 40 walihamishwa kutoka kwenye nyumba zao kutokana na janga hilo.

Kimbunga hicho, kilichofikia mwendo kasi wa kilomita 150 kwa saa, kiliua watu 2 jana, na wavuvi 26 walipotea kwenye boti iliyozama kutokana na upepo.



from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2HNafHH

No comments