Breaking News

Uingereza kuongeza vikwazo vya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona wiki ijayo

 


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema nchi hiyo itaweka vikwazo vikali kwa wakazi wake wiki ijayo kama sehemu ya kuzuia ongezeko la maambukizi yanayoongezeka ya virusi vya corona. Haya yanajiri wakati ambapo Uingereza imefikia maambukizi milioni moja ya virusi hivyo hapo jana. 

Maduka yasiyouza bidhaa za lazima pamoja na maeneo ya kustarehe yatafungwa kuanzia Alhamis hadi Disemba 2. 

Baa pamoja na migahawa itafungwa pia huku migahawa ikiruhusiwa kutoa huduma za kuwasilisha vyakula kwa wateja wao. 

Shule pamoja na taasisi zengine za elimu zitaendelea kutoa huduma zake. Johnson amesema bila hatua kali kuchukuliwa basi kiwango cha watu wanaofariki kutokana na virusi hivyo huenda kikaongezeka. 

Waziri Mkuu huyo wa Uingereza amesema ameamua kuchukua hatua hizo baada ya nchi zengine za Ulaya kama Ujerumani, Ufaransa na Ubelgiji kuongeza vikwazo.




from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3jMvRkz

No comments