DKT. MPANGO AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI KUACHA KUTUMIA NAFASI ZA KUHARIBU MAZINGIRA.

  Makamu wa Rais Dk. Philip Isdori Mpango 

Na Mwandishi Wetu 

Makamu wa Rais Dk. Philip Isdori Mpango  amewataka viongozi ambao wanatumia nafasi zao na  maslaahi ndio wamekuwa  wakichangia uharibu wa mazingira kwa asilimia kubwa taratibu zitafuatwa ni pamoja kupewa familia 12 zinazoharibu mazingira yetu

Dk.Philip Mpango ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi , mazingira na Utunzaji wa Vyanzo vya Maji lililoandaliwa na Kituo cha Wanahabari, Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA)  lililofanyika  mkoani Iringa.




Dk. Mpango aliongeza kwa kusema "Lazima mazingira yapone na mazingira yabaki salama, viongozi wenye maslahi na kuweka rehani  ya watanzania hawatakiwi" 

Mpango amesema hayupo  tayari kuona  athari kubwa zinarudi kwa wananchi, na hivyo inatakiwa ushirikiano hasa kutoka katika serikali kuu wananchi, vyama vya siasa, vyombo vya habari, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla na kuongeza kuwa kwa ushirikiano huo anaamini Nchi itashinda vita dhidi ya uharibufu  wa mazingira ambao unaendelea.

Ametoa agizo kwa kwa Wakuu wa  Mikoa kuhakikisha wanafanya mikakati ya utunzaji wa mazingira  na pia amesisitiza kulilinda   vyanzo vya maji katika mto  Ruaha kwa nguvu zote, na pia nawakumbusha Wizara husika Mikoa pamoja na Taasisi husika kutekeleza maelekezo yaliotolewa na serikali ikiwa mi pamoja na kuweka alama za mipaka ya Utambuzi katika hifadhi.

Aidha Amewataka viongozi kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa waandishi wa habari katika kutoa elimu kwa jamii juu ya utunzaji wa mazingira.

Post a Comment

Previous Post Next Post