SERIKALI YAOMBWA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU KULIOKOA BONDE LA IHEFU


Bw. Habibu Mchange Mwenyekiti wa Kituo Cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na taarifa MECIRA akiwasilisha taarifa yake kwenye Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji linalofabyika kwenye ukumbi wa Masiti Gangilonga Mkoani Iringa Leo Disemba 19,2022 ambapo Mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdori Mpango.

Serikali imeombwa kufanya maamuzi magumu ili kuokoa chanzo cha maji cha Bonde la Ihefu ambalo limevamiwa na familia 12 na kusababisha chanzo hicho kukauka.

Akizungumza katika Kongamano la Wahariri wa Wadau wa Uhifadhi Mazingira na Utunzaji wa Vyanzo vya Maji leo Desemba 19,2022 mkoani Iringa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema kuwa inasikitisha kuona kwamba uharibifu wa mazingira ni wa kiwango cha juu huku zikiwepo familia 12 zinazojinufaisha kupitia Bonde hilo wakiendelea kukaliwa kimya.

 Deodatus Balile Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile
Amesema kuwa ameamua kutoa taarifa hizo hadharani licha ya ukweli kuwa anajua wapo watu ambao hawatapenda kutokana na ukweli kuwa jambo hilo hata watendaji wa Serikali wanajua ila wamefunga midomo.

Balile amesema kuwa kama wahusika yaani watendaji wa Serikali hawatampatia orodha ya majina ya familia hizo yeye yupo tayari kufanya hivyo ili kunusuru chanzo hicho ambacho kinaendelea kutokea kwa sasa.


Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa familia hizo ndizo zinapaswa kunyweshwa sumu kabla ya wengine kwa sababu wao ndio chanzo kikuu cha uharibifu huo kwa makusudi kabisa wamekuwa wakifanya hivyo kwa manufa yao binafsi.

Awali kabla ya Mwenyekiti Balile alizungumza Mwenyekiti wa wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa Habibu Mchange alimwomba sana Mh Dkt. Makamu wa Rais Dkt Mpango kuwa ili kuokoa na kulinda rasilimali na vyanzo vya maji nchini vita hii inahitaji uchukuaji hatua thabiti bila kumwonea aibu mtu.





Post a Comment

Previous Post Next Post