MUSOMA VIJIJINI WASEMA TAYARI RAIS SAMIA AMESHAWAPA ZAWADI ZA KRISMASI
#KAZIINAONGEA
Utoaji wa Huduma za Afya ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini unaoendelea kuboreshwa umetazamwa na wananchi wa jimbo hilo kama zawadi ya Krismasi iliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwao.
Uboreshaji wa Huduma za Afya kwenye vijiji vyao ulianza Machi 20, 2024 katika Kituo cha Afya cha Kata ya Kiriba ambacho kimejengwa Kijijini Bwai Kwitururu
Oktoba 10, 2024, Kituo cha Afya cha Kisiwani Rukuba, Kata ya Etaro nacho kilizinduliwa
Desemba 6,2024 huduma bora za afya zilianza kutolewa katika Zahanati ya Kijiji cha Nyabaengere.
Kama hiyo haitoshi kabla ya dunia kusheherekea siku kuu ya Christmas Disemba 25,2024 wakazi wa Musoma vijijini watapata zawadi ya uzinduzi wa
Zahanati ya Kijiji cha Nyasaungu ambayo itaanza kutoa Huduma za Afya Disemba 20,2024 na Disemba 23,2024
Kituo cha Afya Makojo kitaanza kutoa Huduma za Afya.
Maboresho hayo yamewafanya wananchi wa eneo hilo kuishukuru sana Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapatia zawadi kubwa za Krismasi ya mwaka huu!
Maboresho hayo yanazifanya huduma za Afya katika jimbo hilo lenye Kata 21 zenye Vijiji 68 zinatolewa kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya, Vituo vya Afya vitano, Zahanati 24 za Serikali na binafsi nne.
Aidha kuna ujenzi wa Zahanati mpya 17 na wanavijiji wanaendelea na ujenzi wa zahanati za vijiji vyao.
Baadhi zahanati hizo tayari zimeanza kupokea michango mikubwa ya fedha kutoka Serikali Kuu
Pia kumekuwa na uzinduzi wa utoaji wa Huduma za Afya kwenye Zahanati mpya ya Kijiji cha Nyabaengere, Kata ya Musanja.
*#KAZIINAONGEA*
MUSOMA VIJIJINI WASEMA TAYARI RAIS SAMIA AMESHAWAPA ZAWADI ZA KRISMASI
Reviewed by Tanzania Yetu
on
December 16, 2024
Rating: 5
Reviewed by Tanzania Yetu
on
December 16, 2024
Rating: 5
.jpg)
No comments