DC MAGIRI AZITAKA SEKTA BINAFSI KUAJIRI WAFANYAKAZI NA KUTOA FURSA ZA KUJIUNGA NA VYAMA

Wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi wakiwa katika uwanja wa majimaji Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakati wa maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Peres Magiri ambae ni mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kanali Ahmed Abbas akizungumza na wafanyakazi uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma

Maandamano ya kutembea kwa miguu kuelekea uwanja wa Majimaji ambako maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ndiko yalikofanyika

Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa PeresMagiri, ambaye amekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas, ameitaka sekta binafsi kushirikiana na serikali katika kuwaajiri wafanyakazi wapya ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.
Magiri ametoa wito huo leo katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Uwanja wa Majimaji, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Katika hotuba yake, Magiri amewasisitiza viongozi wa taasisi na mashirika mbalimbali kuhakikisha wanawapa wafanyakazi wao nafasi ya kujiunga na vyama vya wafanyakazi.
Amesema kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa kikwazo kwa wafanyakazi wanaotaka kujiunga na vyama hivyo, hasa wale wanaositasita, jambo ambalo linaathiri juhudi za kulinda na kutetea haki za wafanyakazi.
Maadhimisho hayo pia yamehusisha utoaji wa tuzo kwa wafanyakazi bora ambapo Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Songea, Happiness Chemkunde, amechaguliwa kuwa miongoni mwa waliotunukiwa.
Chemkunde amepokea cheti cha heshima pamoja na zawadi ya pesa taslimu shilingi laki tano, kama sehemu ya kutambua mchango wake katika sekta ya elimu.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Chemkunde amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea na jopo lililomchagua, akisema licha ya uwepo wa wafanyakazi wengi wenye sifa, heshima hiyo kwake ni kubwa na itamchochea kuendelea kufanya kazi kwa weledi na bidii.
Amesema zawadi hiyo inaleta hamasa kwa wafanyakazi wengine kuongeza juhudi katika kuwahudumia wananchi na kuleta maendeleo katika jamii.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/ndp1vBs
No comments