Breaking News

NYAMGUMA MAHAMUD AIBUKA MSHINDI HABARI ZA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

 

📌Ni kupitia Tuzo za Uandishi wa Habari za  Samia Kalamu Awards

📌Wizara ya Nishati yatambua mchango wake

📌 Yamzawadia fedha taslimu, jiko linalotumia umeme kidogo, kompyuta mpakato na uniti za umeme za mwaka mmoja

- Mhandisi Mramba asema Tuzo ni kielelezo cha kuunga mkono juhudi za Rais Samia uhamasishaji Nishati Safi ya Kupikia

Nyamguma Mahamud, Mwandishi wa Habari  kutoka Mlimani FM ameibuka kidedea katika Tuzo za Uandishi wa Habari za Samia Kalamu Awards 2025 kupitia kipengele cha habari za Nishati Safi ya Kupikia ambapo Wizara ya Nishati imetambua mchango wake kwa kumpa zawadi mbalimbali ili kuendelea kuhamasisha utoaji wa elimu ya Nishati Safi ya Kupikia.

Hafla ya utoaji wa Tuzo hizo imefanyika jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mohamud amekabidhiwa zawadi zake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Mshindi huyo amekabidhiwa fedha taslimu shilingi milioni tano, kompyuta mpakato, jiko linalotumia umeme kidogo na uniti za umeme za mwaka mzima.

"Tunatambua  masuala aliyoyaandika katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia, kwahiyo tumemzawadia pia jiko la umeme la kisasa linalotumia umeme mdogo pamoja na umeme wa kutumia nyumbani kwake kwa mwaka mmoja," amesema Mha. Mramba

Amesema Tuzo ya Nishati Safi ya Kupikia ni kielelezo cha  kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika  kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Samia Kalamu Awards  imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa na kaulimbiu ya "Uzalendo Ndio Ujanja'



No comments