Breaking News

MCHUNGAJI HANANJA AISHAURI SERIKALI KUFUNGA MAKANISA YASIYOFUTA TARATIBU

NA MWANDISHI WETU

MCHNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Richard Hananja ameishauri Serikali kufunga makanisa yote yanayokiuka taratibu za usajili wa makanisa hayo.

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 9, 2025 jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la hivi karibuni la Msajili wa Jumuiya za Kiraia nchini kulifutia usajili wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa madai ya kwamba Askofu wa Kanisa hilo Josephat Gwajima amekuwa akitoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuchoonganisha Serikali na wananchi.

Mchungaji Hananja ameunga mkono Serikali kulifutia usajili Kanisa hilo kwa kusema kuwa Madhabahu siyo mahali pa kutumia kutukana wala kuzomeana, na kueleza kuwa kitendo alichofanya Askofu Gwajima kupitia madhabahu ya kanisa lake ni kinyume na taratibu za usajili wa makanisa.

"Mimi nashauri Serikali, kwa makanisa yote yanayokiuka taratibu piga pini, kama umefuata taratibu za kidunia za kujisajili, fuata taratibu," amesema Mchungaji Hananja.

Amesisitiza kuwa kitendo alichokifanya Askofu Gwajima hakikuwa sawa kutumia madhabahu kujibishana na mamlaka huku akitambua kuwa yeye ni kiongozi yaani Mbunge wa Jimbo la Kawe kadhalina MNEC wa Chama cha Mapinduzi jambo ambali linamfanya kumfikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa urahisi na kuweza kutoa ushauri wake bila kutoka hadharani.

"Gwajima ana nafasi kubwa ya kutoa maoni yake, si ungi mkono vitendo vya utekaji na mauaji hata Bibilia inakataa vitendo hivi, lakini inapaswa kutumia njia sahihi ya kushauri, kila mtu akisema kwa namna yake hatutafika, inatakiwa kushughulika na hili kwa hekima," amesema Mchungaji Hananja na kuongeza,

"Gwajima ni MNEC na ana nafasi kubwa bungeni, hivyo ana nafasi ya kuwa karibu na Rais, kiongozi mkubwa wa nchi. Gwajima ana kutana na Rais wakati wowote, hivyo hapaswi kusema kama mtu wa kawaida bali alitakiwa kusema kama kiongozi kwani ameapa kulinda Katiba na kutunza siri za nchi, hakupaswa kutumia Madhabahu kusema hayo,".

Akizungumzia kuhusu watu kuhoji kwanini Kanisa lifungiwe badala ya kutafuta Askofu Gwajima peke yake, Mchungaji Hananja amesema kuwa Serikali iko sahihi kwasababu Kanisa kwasababu ndiyo taaisi iliyosajiliwa na Serikali na sio mtu binafsi.


Hata hivyo Mchungaji Hananja amesema kuwa kukosoa sio tatizo bali tatizo ni namna ya kukosoa kwamba kukosoa kunapaswa kuwa kwa adabu na sio kwa kutukana na kuzomea.

Ametoa wito kwa viongozi wa Dini na Watanzania kulinda na kutunza amani iliyopo nchini, kwani ikitoweka nchi itasambaratika, hata hivyo ametoa wito kwa viongozi wa dini na Serikali kukutana na kufanya mazungumzo kwa mustakabali wa Taifa.


No comments