Breaking News

RC MRINDOKO AAGIZA HALMASHAURI KUNUNUA MASHINE ZA KURUTUBISHA CHAKULA


Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mhe. Mwanamvua Mrindoko ameziagiza halmashauri zote mkoani hapa kufanya tathmini ya kina itayoonyesha maeneo yenye uhitaji wa haraka wa mashine za kurutubisha chakula kwa lengo la kuboresha  hali ya lishe kwenye jamii.

Agizo hilo amelitoa Juni 10,2025 wakati akifunga kikao cha wadau wa lishe mkoani Katavi ambapo ambapo amewataka kufanya tathimini ya haraka ndani ya mwezi mmoja ziweze kununua mashine na kuzisimamia zifanye kazi ya kuongeza virutubishi kwenye chakula na mafuta ya kula.

"Utafiti wa awali utakaowezesha kujua hali ipo vipi, tunataka kufikia wapi na katika kipindi gani na maeneo gani yanahali mbaya,hali ya kati na maeneo gani hayana hali mbaya kupitia watoto waliopo mashuleni na kwenye kliniki, vituo vya afya na hospitali kwa namna itakavyoonekana kitaalamu inafaa,"

Mhe. Mrindoko ameagiza utafiti huu uweze kufanyika haraka ili kujua hali halisi ya udumavu iwezeshe kupanga vizuri mikakati ambayo itawezesha kufika kwa haraka eneo ambalo litaonekana na udumavu pia amewataka wananchi kuunga mkono jitihada hizi na mikakati mbalimbali itakayowezesha kuondokana na udumavu na kuboresha hali ya lishe kwa jamii nzima.
 
Aidha amemuagiza katibu tawala wa mkoa kusimamia mikakati ya lishe na kuongeza kipengere kinachohusiana na upatikanaji wa mashine hizo katika halmashauri zote na kwenye maeneo muhimu kama vile vitongoji mitaa shule za msingi na sekondari ili jamii nzima iweze kupata nafasi ya kupata virutubisho.



from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/k6uf4QB

No comments