Breaking News

TEITI yaweka wazi ripoti ya 15 ya mwaka wa fedha 2022/2023






TANZANIA ikiwa ni nchi mwanachama wa EITI imeendelea kutekeleza Matakwa ya Kimataifa ya EITI ambapo kila mwaka nchi mwanachama wa Asasi ya EITI inatakiwa kuweka wazi Ripoti za ulinganishi wa mapato ya Serikali na malipo ya Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia hayo yamesemwa na Bw. Erick Ketagory - Kaimu Meneja Kitengo cha Uwazi na Uwajibikaji kutoka Taasisi ya TEITI katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

Amesisitiza kwamba, katika kutekeleza Matakwa hayo, Taasisi inayosimamia utekelezaji wa Shughuli za EITI hapa nchini imeweka wazi ripoti ya TEITI kwa mwaka wa fedha 2022/3023. Ripoti imeandaliwa na Wataalam wa ndani ikiwa ni mara ya pili wataalam wa ndani kuandaa ripoti hizo za TEITI.

Aidha, ameeleza kuwa Pamoja na masuala mengine, ripoti hiyo imelinganisha malipo ya Kampuni 47 za madini,mafuta na gesi asilia na mapato ya serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Kwa upande mwingine, ripoti ya 15 ya TEITI imeweka wazi taarifa mbalimbali kulingana na matakwa ya kimataifa ya EITI pamoja na Sheria ya TEITA, 2015 ikuwemo hatua iliyofikia kama nchi katika takwa la uwekaji wazi wa mikataba, taarifa za ajira katika sekta ya uziduaji, taarifa kuhusu uwekaji wazi wa majina ya wamiliki wa kampuni katika sekta ya uziduaji, takwimu za uzalishaji wa rasilimali madini, mafuta na gesi asilia. Ripoti hiyo imetoa mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha sekta ya uziduaji nchini.

Ripoti hii inapatikana katika Tovuti ya Taasisi ya TEITI kupitia:
https://www.teiti.go.tz/storage/app/uploads/public/685/e74/0d3/685e740d3bc78880361428.pdf

No comments