Breaking News

MALI ZA UMMA NA BINAFSI ZIMECHOMWA, HAYAKUWA MAANDAMANO—ZILIKUWA VURUGU




Na Mwandishi wetu, DAR

Samwel Salum, mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam, amelaani vikali matukio ya Oktoba 29 akieleza kuwa hayakuwa maandamano halali bali vurugu zilizoleta uharibifu mkubwa wa mali za umma na watu binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Samwel amesema vitendo hivyo havikuwa na lengo la kutoa ujumbe kwa Serikali bali vilichochewa na nia ovu ya kuharibu, kujeruhi, na kuathiri uchumi wa Taifa.

“Maandamano ya kweli huwa na hoja au ujumbe unaoeleweka kwa mamlaka husika, lakini haya ya Oktoba 29 yalikuwa vurugu tupu. Watu wamepoteza mali zao, maduka yamechomwa, na shughuli za kiuchumi zimesimama,” amesema Samwel kwa masikitiko.

Ameongeza kuwa vitendo vya namna hiyo vinapaswa kulaaniwa na Watanzania wote wanaopenda amani, akisisitiza kuwa hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana katika mazingira ya machafuko.







from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/fsnLh25

No comments