Breaking News

TUITUMIE MITANDAO KUTAFUTA PESA, SIO KUFANYA UCHOCHEZI- VIJANA WAFUNGUKA



Na Mwandishi wetu, Dar

Wananchi wa Tanzania wameaswa kuitafuta na kuilinda amani kwa wivu mkubwa badala ya kuendekeza machafuko na kutumia mitandao ya kijamii kwa uchochezi.

Kauli hiyo imetolewa leo, Novemba 10, 2025, jijini Dar es Salaam wakati kundi la vijana lilipozungumza na waandishi wa habari kuhusu athari za maandamano ya vurugu yaliyotokea Oktoba 29, 2025, na kusababisha simanzi kubwa nchini.

Vijana hao wamesema ni muhimu kwa kizazi cha sasa kutambua thamani ya amani kama nguzo kuu ya maendeleo ya taifa, wakisisitiza kwamba uchochezi na usambazaji wa taarifa za upotoshaji mtandaoni huongeza migawanyiko na chuki miongoni mwa wananchi.

Wameitaka Serikali, viongozi wa dini na wazazi kushirikiana katika kutoa elimu ya uraia na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ili kuzuia matukio ya vurugu kama yaliyojitokeza mwishoni mwa Oktoba.

Kwa mujibu wa vijana hao, “amani ni urithi wa thamani ambao kila Mtanzania anapaswa kuutunza,” wakisisitiza kuwa ni jukumu la wote kuhakikisha Tanzania inaendelea kubaki nchi ya utulivu na umoja.




from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/slCtQfa

No comments